Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na baadhi ya viongozi kuelekea eneo la tukio kukagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Mpiji lililokatika kutokana na Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini.
Nguzo za umeme zikiwa zimeinama baada ya kuzidiwa nguvu na maji hayo yaliyobomoa daraja.
Malori yakimwaga vifusi vya Mawe kwenye daraja hilo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa maelekezo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Eng. Mussa Ibrahim Iombe, wakati alipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Mpiji lililokatika kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini.Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mecky Sadick




Hakuna maoni :
Chapisha Maoni