Kamanda Muhidin Maalim Gurumo akipeana mkono na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Mwanamuziki mkongwe nchini Muhidin Maalim Gurumo, alimaarufu kwa mashabiki wake "Kamanda" amefariki dunia leo mchana katika hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu.
Gurumo mmoja wa wanamuziki mwenye historia kubwa katika muziki wa dansi wa Tanzania, alistaafu baada ya miaka 53 ya kusimama jukwaani akiwa na Bendi ya Msondo Ngoma Music Band "baba ya muziki", zamani ikifahamika kama Nutta Jazz, Juwata Jazz Band na baadaye Ottu kabla ya kuitwa Msondo na kumilikiwa na wanamuziki wenyewe.
Meneja wa Msondo Ngoma, Said Kibiriti amesema msiba upo Tabata External Makuburi jijini Dar es Salaam, na maziko yatafanyika kesho mchana Masaki Kisarawe mkoa wa Pwani
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni