Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, leo ameongoza maelfu ya waislamu katika mazishi ya mwanachuoni Sheikh Khamis Makungu Haji wa Ndijani, Mkoa wa Kusini Unguja.
Kwa mujibu wa mjukuu wa marehemu bw. Abdallah Ameir, Sheikh Makungu amefariki akiwa na umri wa zaidi ya miaka mia moja.
Bw. Ameir amesema mbali ya kwamba sheikh Makungu alikuwa mwanazuoni wa kutegemewa katika Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar na nje ya Zanzibar, pia alikuwa akijushughulisha na masuala ya tiba za ki-sunna ambapo waislamu kutoka maeneo tofauti walikuwa wakimtumia kwa masuala hayo.
Mapema akizungumza katika msiba huo, Mkuu wa Chuo cha Kiislamu Zanzibar Dkt. Muhidin Ahmed Khamis, amesema pengo aliloliwacha mwanazuoni na mtabibu huyo haliwezi kuzibika mara moja.
Dkt. Muhidin amewahimiza waislamu kusoma kwa bidii ili kuweza kuyaendeleza mambo mema yanayoachwa na wanazuoni.
Hassan Hamad, OMKR.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni