Makamu
wa rais wa Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal, Waziri wa Ujenzi Dk.
John Magufuli pamoja na RPC Suleman Kova wamenusurika katika ajali
leo baada helkopta waliyokuwa wamepanda kupata hitilafu wakati ikiruka
Ukonga kwenda kuangalia athari zilizosababishwa na mvua Jijini Dar es
Salaam.
Wengine
waliokuwemo ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Mecky Sadiki pamoja
na wajumbe wa kamati ya maafa, ambapo hakuna mtu yeyote aliyejeruhiwa
katika ajali hiyo na walipelekwa hospitali kuchunguzwa iwapo wamepata
madhara na kuruhusiwa.
Tukio hilo
limetokea leo Jijini Dar es Salaam katika uwanja wa ndege wa jeshi wa
Ukonga majira ya saa tano asubuhi, ambapo viongozi hao walipokuwa
wakijiandaa kupaa na helkopta hiyo na ndipo ilipopata hitilafu baada
ya kuruka juu kidogo na kuanguka.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni