Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
akipokewa na Mkuu wa Wilaya ya Bahi Ndugu Betty Mkwasa mara baada ya
kuwasili mjini Bahi kushiriki mkwenye sherehe ya uzinduzi wa
uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi. (Picha na John Lukuwi)
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya
Wanawake na Maendeleo, Mama Salma Kikwete akiwasalimia wanafunzi na
wananchi wa Bahi waliohudhuria sherehe ya uzinduzi wa saratani ya
shingo ya kizazi mjini hapo
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama
Salma Kikwete akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa kampeni ya
kutokomeza saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake wa Wilaya ya
Bahi
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
akionyesha vifaa mbalimbali vinavyotumika na madaktari wakati wa
kuwapima wanawake ili kufahamu kama wana maambukizi ya saratani ya
shingo ya kizazi wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo wilayani Bahi
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
akiwahutubia mamia ya wananchi wa wilaya ya Bahi muda mfupi kabla ya
kuzindua rasmi kampeni ya upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi kwa
wanawake katika wilaya ya Bahi mkoani Dodoma.





Hakuna maoni :
Chapisha Maoni