Rais Uhuru
Kenyatta wa Kenya yupo Jijini London Uingereza kumuunga mkono mkewe
Margaret Kenyatta wakati akiweka historia ya kushiriki mbio za
marathoni zinazofanyika katika jiji hilo hii leo.
Ndege iliyombeba
rais Kenyatta na watu walioambatana nae ilitua jana kwenye uwanja wa
Heathrow na kulakiwa na maafisa wa Uingereza pamoja na balozi wa
Kenya nchini humo, Ephraim Ngare.
Wanariadha wapatao
elfu 35 watakimbia mbio hizo kupitia maeneo muhimu ya Jiji la Landon
katika mbio hizo ambazo hii ni mara ya 34 kufanyika.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni