Nguli wa muziki wa dansi nchini Tanzania, Muhidin Maalim Gurumo atazikwa leo katika makaburi ya kijijini kwao Masaki wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani majira ya mchana.
Kabla ya msafara kuanza kuelekea Masaki kwa maziko, Gurumo ataagwa na mashabiki na wapenzi wa muziki wa dansi nyumbani kwake Mabibo External jijini Dar es Salaam, mwili wake unatarajiwa kufikishwa nyumbani kwake saa tatu asubuhi ukitokea Hospital ya Muhimbili ulikohifadhiwa.
Muhidin Gurumo amefariki juzi jumapili katika hospitali ya Muhimbili baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa moyo.
Mbali ya kuiimbia na kuiongoza Msondo Ngoma kwa mafanikio makubwa, Gurumo pia alipata kuziimbia bendi mbalimbali ikiwemo Ddc Mlimani Park na Orchestra Safari Sound ( OSS )

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni