Nahodha wa kivuko cha Korea Kusini kilichozama jumatano amekamatwa na polisi baada ya kugundulika kuwa wakati kivuko hicho kilipoanza kuzama alikuwa ni mmoja kati ya watu waliotoka ndani ya kivuko hicho wa kwanza bila kutoa msaada kwa abiria wake.
Nahodha huyo Leen Joon-Seok mwenye miaka 68 ( pichani juu akishuka ) ameshtakiwa kwa kuwatelekeza abiria wake na kusababisha vifo 28 na mpaka sasa bado watu 270 hawajaokolewa.
Kivuko hicho kilikuwa na abiria 470 wengi wao wakiwa wanafunzi na kilikuwa kinaelekea kusini mwa kisiwa cha Jeju.
Lee Joon- Seok ( katikati ) akifikishwa katika mahakama ya Mokpo kusini mwa Seoul hii leo kujibu mashitaka yanayomkabili.
Shughuli za uokoaji zikiendelea eneo kilipozama kivuko hicho
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni