.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 21 Aprili 2014

NDEGE NYINGINE YA MALAYSIA IKIWA NA ABIRIA 159 YAPATA HITILAFU ANGANI, ABIRIA WATOKA SALAMA

 Ndege ya shirika la ndege la Malaysia Boeing 737 iliyokuwa na abiria 159 imelazimika kutua kwa dharura muda mfupi baada ya kuruka kutoka Kuala Lumpur kuelekea Bangalore India. 

Ndege hiyo namba MH 192 ililazimika kuzunguka angani kabla ya kuruhusiwa kutua tena Kuala Lumpur baada ya kutokea hitilafu katika mfumo wake wa gia muda mfupi baada ya kuruka kutoka uwanjani hapo. 

Safari kutoka Kuala Lumpur kwenda Bangalore inasadikiwa kuwa dakika 90, lakini abiria iliwalazimu kukaa angani kwa zaidi ya saa nne wakizunguka anga la Kuala Lumpur wakisubiria mamlaka husika kuruhusu ndege hiyo kutua kwa dharura baada ya kuhakikisha uwanja upo salama na tayari kwa ndege hiyo kutua tena
Waziri wa Uchukuzi wa Malaysia, Hishammuddin Hussein ( mwenye kofia ) akiongea na abiria waliokuwa katika ndege hiyo baada ya abiria wote kutoka salama

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni