.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 24 Aprili 2014

NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA ULAYA, REAL MADRID YAIZAMISHA BAYERN MUNICH

 Timu ya soka ya Real Madrid ya Hispania imeanza vyema harakati zake za kutaka kucheza fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya, baada ya usiku wa kuamkia leo kuitandika Bayern Munich toka Ujerumani kwa bao 1-0 katika mchezo mkali wa nusu fainali ya ligi hiyo uliochezwa katika uwanja wa Santiago Bernabeu. 
 Katika mchezo huo uliokuwa na ushindani mkali, alikuwa ni Karim Benzema aliyewanyanyua mashabiki wa Real Madrid waliofurika uwanjani hapo baada ya kuifungia bao hilo muhimu kunako dakika ya 19 ya kipindi cha kwanza cha mchezo, bao ambalo lilidumu hadi dakika 90 zinamalizika.
Mchezo huo uliochezeshwa na mwamuzi Howard Webb toka Uingereza, ulishuhudia kila timu ikicheza kwa kiwango cha hali ya juu na kushambuliana kwa zamu. Timu hizo zitarudiana wiki ijayo katika uwanja wa Allianz Arena huko Ujerumani
KIJANA POLE NDIO MCHEZO!! Kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti akimkumbatia kocha wa Bayen Munich, Pep Guardiola baada ya mchezo huo

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni