.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 17 Aprili 2014

REAL MADRID YATWAA KOMBE LA COPA DEL REY, YAICHAPA BARCELONA 2-1

 Mshambuliaji mahiri wa Real Madrid, Gareth Bale akiifungia timu yake bao la pili nala ushindi kunako dakika ya 85 ya mchezo huo wa fainali ya kuwania kombe la Copa Del Rey dhidi ya Fc Barcelona na kutwaa ubingwa huo, mchezo uliochezwa usiku wa kuamkia leo. 

Katika mchezo huo, Madrid ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Di Maria dakika ya 11 ya mchezo, bao ambalo lilidumu hadi kipindi cha kwanza kinamalizika. 

Kipindi cha pili Barcelona walikuja juu na kufanikiwa kusawazisha dakika ya 68 kupitia kwa Bartra kabla Bale kuzamisha jahazi la Barcelona kwa kufunga bao safi dakika ya 85
              Raha ya kufunga bao ni kushangilia, Gareth Bale akikimbia kwa furaha
 Bale akiruka kwa furaha mbele ya mashabiki wa Real Madrid baada ya kufunga bao la pili nala ushindi
Nahodha wa Madrid, mlinda mlango Iker Casillas akinyaynyua juu kwa furaha kombe la Copa Del Rey

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni