.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 18 Aprili 2014

VIJANA WENYE SILAHA WAVAMIA KAMBI YA UN NCHINI SUDAN KUSINI NA KUUA RAIA



Makumi ya raia waliohifadhiwa katika kambi ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini katika Mji wa Bor wameuwawa baada ya kushambuliwa na vijana wenye silaha.

Afisa Mwandamizi wa Umoja wa Mataifa Toby Lanzer anayeongoza watumishi wa umoja huo Sudan Kusini, amesema vijana hao walivunja geti la kambi hiyo na kuanza kufyatua risasi kwa raia walioomba hifadhi.

Maafisa wa Umoja wa  Mataifa wanaolinda kambi hiyo yenye kuhifadhi raia wapatao 5,000, walijibu mapigo na kufanikiwa kuwalazimisha vijana hao wenye silaha kukimbia.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni