John Kardinali Njue
Viongozi wa dini ya Kikristo nchini
Kenya na jumuiya ya wafanyabiashara wa Eastleigh, Jijini Nairobi
wameiomba serikali kutumia ubinadamu katika msako wake dhidi ya
watuhumiwa wa ugaidi pamoja na wahamiaji haramu nchini.
Akiongea katika mkutano wao wa pamoja
katika Kanisa la Watakatifu la Jijini Nairobi, John Kardinali Njue,
amevipongeza vyombo vya ulinzi kwa jitihada za kukabiliana na
uhalifu, na kutoa wito viheshimu utu na uhai katika operesheni zake.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni