Chifu amejeruhiwa vibaya nchini Kenya
baada ya watengenezaji pombe za kienyeji kuanzisha vurugu,kumpiga na kumjeruhi kwa kumkata na
kitu chenye makali kwenye paji la uso na kwenye mkono.
Chifu Ezekiel Karanja wa eneo la
Kasarani amelazwa katika kituo cha afya cha Elburgon, baada ya
kushambuliwa na vijana kwa madai ya kuchochea wanakijiji kuvamia
nyumba iliyohifadhi pombe haramu ya chang'aa (gongo) muda mfupi baada
ya kuletwa.
Vijana hao walimvamia Chifu Karanja,
ambaye alienda katika nyumba hiyo iliyotelekezwa akiwa peke yake.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni