.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 13 Mei 2014

MO FARAH ATANGAZA KUKIMBIA MBIO ZA JUMUIYA YA MADOLA HUKO GLASGOW

Mwanariadha wa Uingereza aliyetwaa medali mbili za mbio za Olimpiki Mo Fraha atashiriki mbio za mwaka huu za michuano ya Jumuiya ya Madola zitakazofanyika huko Glasgow.

Farah, alishika nafasi ya nane katika mbio za marathoni za London mwezi Aprili alikuwa hajaamua iwapo atakimbia mbio za Glasgow.

Kocha wake Alberto Salazar, alimshauri Farah kutokimbia tena hadi michuano ya Olimpiki ya Rio 2016.

Umamuzi huo wa Mo Farah umeongeza matumaini kwa waandaji wa michuano hiyo, kutokana na mwanariadha Muingereza Jessica Ennis-Hill kutoshiriki kutokana na kutarajia kujifungua wakati Mjamaica Usain Bolt akiwa bado hajathibisha kushiriki.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni