Mshambuliaji hatari wa Liverpool Suarez akimwaga chozi
Liverpool imevurunda na kujikuta
ikiruhusu kufungwa mabao matatu ndani ya dakika 11 licha ya kuanza
kwa kuongoza kwa mabao matatu kwa bila kwa muda mrefu katika mchezo
wake na Crystal Palace ulioisha kwa sare ya mabao 3-3.
Kwa sare hiyo Liverpool inayonolewa na
Brendan Rodgers imejikuta ikiharibu mahesabu ya kutwaa ubingwa wa Ligi
Kuu ya Uingereza baada ya kupokonywa ushindi jana katika dakika za
mwisho na Crystal Palace katika sare hiyo.
Katika mchezo huo Liverpool ilipata bao
la kwanza kupitia kwa Allen katika dakika ya 18, Sturridge dakika ya
53 na Luis Suarez dakika ya 55, ambapo mbao ya Crystal palace
alifungwa na Delaney dakika ya 79, Gayle dakika ya 81 na 88.
Steven Gerrard akiwa hoi
Daniel Sturridge akiwa haamini kilichotokea



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni