Beki wa kulia wa Gor Mahia Solomon
Nasio anatafuta msaada wa matibabu ili kuweza kupatiwa tiba na
kurejea tena dimbani, baada ya kuonekana kama timu yake imeamua
kumtelekeza.
Nasio alivunjika mshipa wa pua mwaka
jana katika mchezo ambao Gor ilishinda mabao 2-1 dhidi ya timu ya
Karuturi huko Naivasha.
Mchezo wake wa mwisho na Gor Mahia
ulikuwa ni Machi 30, mwaka huu ambapo Gor ilifungwa mabao 2-1, na
Nasio alitolewa baada ya pua yake kuanza kutoa damu.
Na sasa beki huyo mwenye umri wa miaka
28, anahitaji msaada wa kiasi cha shilingi laki moja na nusu ya Kenya
ili awezekufanyiwa upasuaji puani ili kutibiwa tatizo lake.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni