Mwandishi wa habari na mpiga picha raia wa Ufaransa, Camille Lepage ameuawa huko Jamuhuri ya Afrika ya Kati alikokuwa akifanya shughuli zake.
Mwili wa mwandishi huyo uligunduliwa baada ya askari wa kikosi cha kulinda amani cha Ufaransa waliokuwa doria kulisimamisha gari lililokuwa linaendeshwa na wafuasi wa kundi la Anti Barraka katika mkoa wa Bouar.
Mwandishi huyo amekuwa akifanya kazi zake Afrika ya Kati baada ya kuondoka Sudan Kusini July 2012

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni