.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 14 Mei 2014

WACHIMBAJI MADINI 201 WAMEKUFA BAADA YA KUTOKEA MLIPUKO KATIKA MACHIMBO UTURUKI

Zaidi ya wachimba madini 201 wamekufa na wengine 200 wamekwama chini ya Ardhi baada ya mlipuko wa moto katika machimbo ya makaa ya mawe katika jimbo la Manisa Magharibi mwa nchi ya Uturuki.

Waziri wa Wizara ya Nishati nchini humo Bw. Taner Yildiz amesema watu 787 walikuwa ndani ya mgodi huo wakati hitilafu ya umeme ilipotokea na kusababisha mlipuko huo.

Ndugu jamaa na Marafiki wa wachimbaji hao wamekusanyika katika eneo la tukio ambalo ni zaidi ya kilometa 450 kutoka mji mkuu wa nchi hiyo Ankara.

Waokoaji wamefanyakazi usiku mzima kujaribu kuokoa waliosalia chini ya Ardhi katika ajali hiyo mbaya, ambapo ni wachimbaji hamsini tu waliookolewa.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni