Jaji anayesikiliza kesi ya mauaji
inayomkabili Oscar Pistorius ameagiza mwanariadha huyo kufanyiwa
tathimini ya akili yake.
Jaji huyo amesema ushahidi wa mtaalam
wa akili uliotolewa mahakamani hauwezi kubadilishwa hivyo uchunguzi
wa kina unabidi ufanywe juu ya afya ya akili yake.
Waendesha mashtaka walitoa hoja kuwa
ushahidi wa mtaalam wa akili uliodai kuwa Pistorius anatatizo la kuwa
na hofu tangu akiwa mtoto, unapaswa kuthibitishwa kitabibu, wakati
upande wa utetezi ukipinga kwa nguvu Pistorius kupimwa akili yake.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni