Siku ya 28 ya kesi ya mwanariadha
mlemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius imeshuhudia mahakama
ikielezwa kuwa marehemu Reeva Steenkamp huenda alikula chakula chake
cha mwisho usiku alipouwawa na mpenzi wake huyo.
Shahidi Christina Lundgren, mtaalam wa
mwili wa binadamu ameelezea namna tumbo la binadamu linavyoweza
kuonekana likiwa halina chakula baada ya kula.
Amesema tuhuma za kuwa kulikuwa na
malumbano kuwa tumbo la Steenkamp lilikuwa na chakula ama tupu wakati
Pistorius alipomua zilijengwa katika uvumi mtupu.
Pistorius amekanusha kumuua kwa
makusudi mpenzi wake Steenkamp Februari 14 mwaka jana.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni