Mwanaume mmoja raia wa Tanzania jana
amekamatwa kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta
Jijini Nairobi akisafirisha dawa za kulevya aina ya cocaine zenye
thamani ya shilingi milioni 1.2 za Kenya.
Mtu huyo aliyetokea Tanga na kuingia
Kenya kupitia Mombasa pia alinaswa na dawa za kulevya aina ya heroine
alizokuwa amezishindilia kwenye njia ya haja kubwa zikiwa na thamani
ya shilingi 105,000 ya Kenya.
Mkurugenzi wa Upelelezi Joseph Ngisa
amesema walimsimamisha Mtanzania huyo na kumshikilia katika uwanja wa
Jomo Kenyatta baada ya kumshuku na kufanikia kutoa kete 16 za cocaine
na keti mbili za heroine.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni