Polisi wa majimbo nchini Brazil
wameanza mgomo kuhusiana na madai yao malipo, na wametishia
wataendelea na mgomo wao huo hata wakati wa fainali za Kombe la
Dunia, mwezi ujao.
Msemaji wao afisa wa polisi Renato
Deslandes, ameviambia vyombo vya habari kuwa karibu asilimia 40 ya
polisi wameanza mgomo huo.
Amesema kuwa mgomo huo utaendelea iwapo
serikali haitaongeza mishahara yao ili kuendana na kiwango cha
mfumuko wa bei kilichopo sasa nchini Brazil.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni