Klabu ya Sevilla imeifunga kwa
mikwaju ya penati Benfica na kutwaa ubingwa wa Ligi ya Uropa katika
mchezo uliochezwa Turin, na kuweka rekodi ya kuchukua kombe hilo mara
tatu katika misimu tisa.
Matokeo hayo yameifanya Benfica,
kushindwa mara saba katika michezo saba ya fainali ligi ya uropa na
kukosa nafasi kulitwaa kombe hilo tangu mwaka 1962.
Mchezaji Kevin Gameiro alifunga
mkwaju wa penati ya mwisho baada ya kipa wa Sevilla, Beto kupangua
mikwaju ya penati ya Oscar Cardozo na Rodrigo, na kufanya matokeo
kuwa mabao 4-2.
Rais wa UEFA Michel Platini akikabidhi kikombe kwa wachezaji wa Sevilla



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni