.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 9 Mei 2014

KOCHA MSAIDIZI HARAMBEE STARS AREJESHWA KAZINI BAADA YA KUFUKUZWA KAZI

                                                              Kocha Adel Amrouche

Mamlaka inayosimamia Soka nchini Kenya imetengua uamuzi wa kocha mkuu wa timu ya Taifa Harambee Stars, Adel Amrouche wa kumtimua kazi msaidizi wake James Nandwa.

Mkutano uliofanyika jana wa maafisa wa shirikisho la soka Kenya umeridhia kumrudisha kazini Nandwa, ambaye tofauti zake na Amrouche zilikuwa zinatishia kuzorotesha maandalizi ya Harambee Stars katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika.

Taarifa iliyotolewa na kikao hicho cha shirikisho la soka imeeleza kuwa ni wajibu wa shirikisho kulinda ajira za wazawa hivyo Nandwa ataendelea kutekeleza majukumu yake ya kusaidia kuinoa Harambee Stars.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni