Kocha wa Harambee Stars ya
Kenya, Adel Amrouche anaamini kuwa Kenya itashiriki michuano ya Kombe
la Mataifa ya Afrika mwaka 2015.
Amrouche amesema Kenya
inataka kucheza michuano hiyo na imejiandaa kwa kila kitu kuhakikisha
kuwa inashiriki michuano hiyo mikubwa ya soka barani Afrika.
Kocha Amrouche ametoa
kauli hiyo katika ujumbe wake kwa waandishi wa habari wakati akikinoa
kikosi cha wachezaji 17 wa Harambee Stars katika uwanja wa mpira wa
Safaricom.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni