.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 7 Mei 2014

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MKUTANO WA MAZUNGUMZO BAINA YA VIONGOZI WA DINI NA WANASIASA KUHUSU UJENZI WA DEMOKRASIA NA AMANI JIJINI DAR


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Mkutano wa siku mbili wa Mazungumzo baina ya Viongozi wa Dini mbalimbali na Wanasiasa kuhusu ujenzi wa Demokrasia, Maendeleo na uimarishwaji wa Amani ulioshirikisha nchi za Afrika na kufanyika kwenye Hoteli ya White Sands, jijini Dar es Salaam, leo Mei 6, 2014. Picha na OMR.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TAnzania,. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akishiriki dua ya pamoja na baadhi ya viongozi wa dini, kutoka (kushoto) ni Katibu Mkuu wa BAKWATA, Sheikh Suleiman Loila, Askofu Dkt. Alex Malasusa na (kulia) ni Sheikh Khamis haji, wakati wa ufunguzi rasmi wa Mkutano wa siku mbili wa Mazungumzo baina ya Viongozi wa Dini mbalimbali na Wanasiasa kuhusu ujenzi wa Demokrasia, Maendeleo na uimarishwaji wa Amani ulioshirikisha nchi za Afrika uliofanyika kwenye Hoteli ya White Sands, jijini Dar es Salaam, leo Mei 6, 2014. Picha na OMR.
 

Baadhi ya wadau wa mkutano huo waliohudhuria, kutoka (kushoto) ni Wilfred Mlay, Dkt. Willibrod Slaa, Hellen Kijo-Bisimba na wengineo wakishiriki dua ya pamoja.
 

                         Askofu Dkt. Alex Malasusa, akizungumza wakati wa Mkutano huo.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni