.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 10 Mei 2014

MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR, BALOZI SEIF AFUNGA MKUTANO WA 12 WA CHAMA CHA MAJAJI WANAWAKE DUNIANI JIJINI ARUSHA

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Mahakama ya Kimataifa Jaji Sanji Mmasenono Monageng Raia wa Jamuhuri ya Botswana akifurahia Tuzo Maalum aliyokabidhiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Majaji Wanawake Duniani Jaji Eusebia Munuo kushoto yake kwenye Tafrija ya Wajumbe wa Mkutano huo iliyofanyika Mkoani Arusha.Pembeni yao kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Chama cha Majaji Wanawake Duniani { IAWJ } anayefanya kazi zake Makuu ya Chama hicho Mjini Washington Marekani Jaji J. Winship.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mh. Mohamed Chande Othman akitoa neno la shukrani kwenye tafrija maalum ya chakula cha usiku iliyoandaliwa kwa ajili ya Wajumbe wa Mkutano wa 12 wa Chama cha Majaji Wanawake Duniani hapo Hoteli ya Mount Meru Arusha.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Mjumbe wa Chama cha Majaji Duniani kutoka Nchini Swatzeland Jaji Sandry kwenye Tarija maalum ya Wajumbe wa Mkutano wa Majaji Wanawake Duniani.
Wajumbe wa Mkutano wa 12 wa Chama cha Majaji Wanawake Duniani wakiserebuka kwenye Ngoma za hali ya juu zilizochaguliwa maalum kuwaburudisha baada ya kumaliza kazi ngumu ya Mkutano wao uliofanyika Mjini Arusha.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni