Marekani imeelezea kuwa utekaji nyara
wanafunzi wa kike zaidi ya 200 uliofanywa na kundi la Boko Haram kuwa
ni suala la ukatili na imesema itasaidia katika kuwakomboa.
Msemaji wa Ikulu ya Marekani Jay Carney
amesema Rais Barack Obama ameshapatiwa maelezo kuwa usalama wa taifa
wa Marekani unafuatilia maendeleo ya tukio hilo la kikatili.
Wanafunzi hao wakike wapatao 250
walitekwa wakiwa shuleni Kaskazini mwa jimbo la Borno tangu Aprili
14.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni