Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro
Nayalandu, akionyesha funguo ya moja kati ya magari matatu aina ya
Land Cruiser, yenye thamani ya Sh. milioni 350, baada ya kupokea
kutoka kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Uhifadhi Wanyamapori Tanzania,
Eric Pasanisi (kulia) wakati wa hafla ya makabidhiano hayo
iliyofanyika jana kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro wakati wa
Kongamano la Kampeni ya kudhibiti Ujangili na kukomesha mauaji dhidi
ya Tembo, Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa
Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, Abdulkarim Shah.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro
Nayalandu, akijaribu kuwasha moja kati ya magari matatu aina ya Land
Cruiser, yenye thamani ya Sh. milioni 350, baada ya kukabidhiwa na
Mwenyekiti wa Taasisi ya Uhifadhi Wanyamapori Tanzania, Eric
Pasanisi, wakati wa hafla ya makabidhiano hayo iliyofanyika jana
kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro wakati wa Kongamano la Kampeni ya
kudhibiti Ujangili na kukomesha mauaji dhidi ya Tembo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro
Nayalandu, akisainiana mkataba wa makabidhiano wa magari matatu aina
ya Land Cruiser, yenye thamani ya Sh. milioni 350, na Mwenyekiti wa
Taasisi ya Uhifadhi Wanyamapori Tanzania, Eric Pasanisi (wa pili
kushoto) wakati wa hafla ya makabidhiano hayo iliyofanyika jana
kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro wakati wa Kongamano la Kampeni ya
kudhibiti Ujangili na kukomesha mauaji dhidi ya Tembo, kushoto ni
Naibu Spika wa Bunge la Jamhri, Job Ndugai (kulia) ni Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii, Mahmoud Mgimwa.
Baadhi ya washiriki wa Kongamano la
Kampeni ya kudhibiti Ujangili na kukomesha mauaji dhidi ya Tembo,
wakiwa katika Kongamano hilo, lililomalizika jan kwenye Hoteli ya
Hyatt Kilimanjaro, jijini Dar Es Salaam.
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dkt.
Reginald Mengi, akichangia mada wakati wa Kongamano hilo,
lililomalizika jana kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro, Jijini Dar es
Salaam.Kongamano hilo lilifunguliwa na Makamu wa Rais Dtk. Mohamed Gharib Bilal.





Hakuna maoni :
Chapisha Maoni