Nyota wa muziki Will.i.am amepatwa na
hasira baada kudaiwa kufukuzwa katika chumba cha daraja la kwanza cha
uwanja wa ndege siku ya Jumamosi, ambacho hutumika kupumzikia watu
mashuhuri.
Nyota huyo wa kundi la Black Eyed Peas
ameandika twitti kadhaa zikililinge shirika la ndege la United,
baada ya kuripotiwa kuambiwa aondoke katika chumba hicho cha watu
maalum, kwa madai kuwa ana kadi feki.
Katika moja ya posti zake zilizoonyesha
kukerewa na kitendo hiyo Will.i.am alitwitti maneno haya:# Shirika la
Ndege la United ni baya. Mimi ni memba na nina kadi ya kuthibitisha
hilo. Lakini wameniambia mimi kadi yangu ni feki na kunitimua kwenye
chumba cha VIP, inasikitisha.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni