.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 6 Mei 2014

MKURUGENZI DART ATOE KESHO RIPOTI YA KINA YA UTEKELEZAJI WA MRADI WA BRT

Tarehe 30 Aprili 2014 nilifanya mazungumzo na wawakilishi wa wafanyakazi kufuatia mgomo uliokuwa unaendelea. Baada ya kuzungumza nao niliwasiliana na uongozi wa Mkoa ambao wafanyakazi walikuwa wanahitaji kukutana nao kufuatia Mkuu wa Mkoa kwenda wakati wa mgomo uliopita na kuahidi kuchukua hatua kuhusu madai yao.

Nilijulishwa kwamba Mkoa ungetuma mwakilishi tarehe 2 Mei 2014 kuwezesha ufumbuzi hatua ambayo ilifanya nisitishe kwenda kutembelea eneo la mgogoro kwa matumaini kwamba mamlaka zinazohusika za Serikali zingewezesha ufumbuzi wa haraka na wa haki.

Hata hivyo, tarehe 5 Mei 2014 ilinibidi nisiondoke kwenda Bunge ili pamoja na mambo mengine niweze kufanya mazungumzo ya karibu zaidi na wawakilishi wa wafanyakazi hao.

Hatua hiyo imenifanya nilibaini kwamba upande wa Serikali na vyombo vyake uliegemea zaidi kwa mkandarasi na mwajiri kampuni ya Starbag kuhusu mgogoro huo wenye athari kwa mradi wa Mabasi ya Haraka (BRT).

Hali hiyo imejidhihirisha kwenye majibu mepesi ya watendaji wa DART waliozungumza na vyombo vya habari jana kuhusu hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa mradi na hali ya mgogoro unaoendelea hivi sasa baina ya Kampuni na wafanyakazi.

Aidha, sijaridhika maelezo yaliyotolewa kuhusu hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa mradi nikilinganisha na mipango ambayo tulielezwa kwa nyakati na katika vikao mbalimbali kati ya mwaka 2011 mpaka 2013.

Katika muktadha huo, natoa mwito kwa Mkurugenzi wa DART kuwasilisha katika Ofisi ya Mbunge Jijini Dar Es Salaam kesho tarehe 7 Mei 2014 Ripoti mbili zenye maelezo ya zaidi na vielelezo vya ziada: Mosi, Juu ya utekelezaji wa mradi mpaka sasa na mwelekeo wa mbele. Pili, kuhusu ushughulikiaji wa mgogoro baina ya Kampuni ya Starbag na Wafanyakazi wa Kampuni hiyo.

Mkurugenzi wa DART asipowasilisha ripoti hizo kesho itanibidi nisitishe kuendelea mazungumzo na wafanyakazi na badala yake niondoke kesho kwenda Dodoma kuihoji Serikali Bungeni.

Kazi ya kwanza niyakwenda kuifanya Bungeni ni kuondoa Shilingi katika Mshahara wa Waziri Mkuu kueleza kutoridhishwa na ufanisi wa DART inayopaswa kwa kushirikiana na Wakala wa Barabara (TANROADS).

Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia DART na Wizara ya Ujenzi kupitia TANROADS zilipaswa kuisimamia Kampuni ya Strabag kwa karibu iweze kutekeleza mradi kwa wakati, kwa kiwango, kwa thamani muafaka ya matumizi ya fedha za mradi (value for money) bila unyonyaji wala ufisadi.

Wenu katika uwakilishi wa wananchi,

John Mnyika (Mb)

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni