.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 14 Mei 2014

MWENDESHA MASHTAKA WA ICC FATOU BENSOUDA ASEMA KESI YA WILLIAM RUTO KUENDELEA LICHA YA VIKWAZO

Kesi iliyopo Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) dhidi ya Naibu Rais wa Kenya William Ruto, itaendelea mbele licha ya kukabiliwa na vikwazo vikubwa, Mwendesha Mashtaka wa Mahakama hiyo Fatou Bensouda amesema.

Bensouda pia amesema anapanga kukutana na katika siku za hivi karibuni na Mwanasheria Mkuu Githu Muigai, kuzungumzia ombi la mahakama la kutaka kuweza kupata rekodi za kifedha za Rais Uhuru Kenyatta.

Alipo ulizwa kuhusu kesi ya Ruto, katika mkutano na waandishi wa habari kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, Bi. Bensouda amesema kunavikwazo vingi kwa mashahidi kukataa kutoa ushahidi baada ya kubadili misimamo yao katika dakika za mwisho.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni