.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 12 Mei 2014

UBINGWA WA LIGI KUU UINGEREZA, RAHA ZARINDIMA ETIHAD STADIUM, HUZUNI YATAWALA ANFIELD STADIUM

 Mshambuliajiwa Manchester City, Sergio Aguero akiwa amenyanyua juu kombe la ubingwa wa ligi kuu Uingereza baada ya kutangazwa mabingwa hapo jana katika uwanja wao wa Etihad Stadium baada ya kuifunga West Ham United mabao 2-0 na kufikisha pointi 86, huku Liverpool ikimaliza ya pili baada ya kuifunga Newcastle mabao 2-1 na kufikisha pointi 84.
 Mashabiki wa Liverpool wakiwa na nyuso za huzuni baada ya timu yao kushindwa kutwaa ubngwa wa ligi kuu Uingereza msimu huu. Ili kuwa mabingwa, Liverpool jana ilipaswa kuifunga Newcastle na wakati huo huo kuiombea Manchester City ifungwe na West Ham United na wala sio kutoka sare kitu ambacho kilishindikana.
 Raha bila kikomo Etihad Stadium baada ya Manchester City kutwaa ubingwa hapo jana.
Huzuni mwanzo mwisho Anfield Stadium kwa mashabiki wa Liverpool baada ya timu yao kushindwa kutwaa ubingwa msimu huu.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni