Wafanyakazi watatu wa usafiri wa umma
maarufu kama matatu nchini Kenya wamesomewa mashtaka ya kuhusika na
mlipuko ya mabasi iliyotokea barabara ya Thika, siku ya jumamosi.
Watuhumiwa hao wamefunguliwa mashtaka
ya kushindwa kuzuia tukio hilo lililosababisha vifo, na kuagizwa
kutoa dhamana ya shilingi milioni 5 ya Kenya kila mmoja na kutoa
vyeti vya mali yenye thamani ya shilingi milioni 5.
Mwendesha Mashtaka alimueleza Hakimu
Mkuu wa Mahakama ya Makadara Emily Ominde kuwa wafanyakazi hao wa
mabasi walishindwa kuwapekua abiria na kutoa fursa ya kupenyezwa
milipuko iliyolipua mabasi.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni