.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 10 Mei 2014

WAZIRI MKUU WA CHINA AWASILI KENYA

Rais wa Kenya, Mh Uhuru Kenyatta ( kulia ) akiwa na mgeni wake Waziri Mkuu wa China Le Keqiang mara alipowasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi jana ijumaa. Kulia mwa Rais, Ni Makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto. 

Waziri Mkuu wa China, Le Keqiang amewasili Nairobi nchini Kenya kwa ziara ya kiserikali ya siku tatu nchini humo. 

Keqiang aliwasili Nairobi usiku wa ijumaa na kupokelewa na mwenyeji wake Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta.

Waziri Mkuu huyo wa China aliyeongozana na mke wake, Mrs Cheng Hong pamoja na ujumbe wa wafanyabiashara zaidi ya 300, atakuwa na mazungumzo na mwenyeji wake Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta na baadaye kusaini miradi mbalimbali ya maendeleo yenye thamani kubwa ya mamilioni ya shilingi. 

Pia Keqiang anatarajiwa kuwa na mkutano na Marais wa nchi nne za Jumuiya ya Afrika Mashariki kesho jumapili May 11' 2014 jijini Nairobi.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni