
Meneja Msaidizi Masoko wa Benki ya Exim Tanzania, Bi Anita Goshashy (Watatu Kushoto) akikabidhi magodoro kwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala, Dkt. Sophinias Ngonyani (Kushoto). Wakishuhudia ni Wafanyakazi wa Benki ya Exim. Benki ya Exim imetoa magodoro 60 katika Wadi ya Wazazi katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki katika kuadhimisha Siku ya Mama Duniani. Wa kwanza kushoto ni Muuguzi Kiongozi Sr. Tuswege Mwamwaja na Kulia ni Muuguzi Mkunga Bi. Marietha Mwageni. (Picha na Mpiga Picha Wetu)

Muuguzi Kiongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala Sr. Tuswege Mwamwaja (wa kwanza kulia) akifafanua jambo kwa wafanyakazi wa Benki ya Exim Tanzania mara baada ya Benki hiyo kukabidhi magodoro 60 katika Wodi ya Wazazi Hospitalini hapo mwishoni mwa wiki katika kuadhimisha Siku ya Mama Duniani. (Picha na Mpiga Picha Wetu)

Meneja Msaidizi Masoko wa Benki ya Exim Tanzania, Bi Anita Goshashy (Watatu Kushoto) akikabidhi magodoro kwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala, Dkt. Sophinias Ngonyani (Kushoto). Wakishuhudia ni Wafanyakazi wa Benki ya Exim. Benki ya Exim imetoa magodoro 60 katika Wadi ya Wazazi katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki katika kuadhimisha Siku ya Mama Duniani. Picha na Mpiga Picha Wetu.

Katibu wa Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim Bi. Erica Mbutu (wakwanza kushoto) na Meneja Msaidizi Msoko wa Benki ya Exim, Bi Violet Bikoche (Wapili Kushoto) wakizungumza na mmoja kati ya kinamama waliojifungua mara baada ya kukabidhi magodoro katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala. Benki ya Exim imetoa magodoro 60 katika Wodi ya Wazazi Hospitalini hapo mwishoni mwa wiki katika kuadhimisha Siku ya Mama Duniani. (Picha na Mpiga Picha Wetu)

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala Dkt. Sophinias Ngonyani (wa kwanza kulia) akifafanua jambo kwa wafanyakazi wa Benki ya Exim Tanzania mara baada ya Benki hiyo kukabidhi magodoro 60 katika Wodi ya Wazazi Hospitalini hapo mwishoni mwa wiki katika kuadhimisha Siku ya Mama Duniani. (Picha na Mpiga Picha Wetu).
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni