Ajali mbaya ya barabarani imetokea maeneo ya Yombo Dovya jijini Dar es Salaam leo asubuhi ikihusisha magari mawili, moja likiwa ni basi dogo la abiria aina ya Toyota Hiace linalofanya safari zake kati ya Tandika na Yombo lililogongana uso kwa uso na gari dogo aina ya Rav 4.
Katika ajali hiyo inaelezewa kuwa dereva wa Toyota Hiace ana hali mbaya sana huku dereva wa Rav 4 naye akiwa amejeruhiwa kiasi.
Wananchi waliojitokeza kutoa msaada kwa abiria waliokuwa ndani ya magari hayo baada ya ajali kutokea.
Askari wa usalama wa barabarani akikagua mazingira yaliyosababisha ajali hiyo.
Wananchi waliojitokeza wakijaribu kuwatoa abiria waliokuwa ndani ya daladala hilo mara tu ajali ilipotokea
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni