Chama cha Riadha Kenya (AK) kimeibua
msuguano na wanariadha pamoja na mameneja wao baada kuwazuia
wanariadha wanne kushiriki Ligi ya Almasi katika muda usio julikana
kutokana na kushuka kwa kiwango chao.
Bingwa wa Dunia Asbel Kiprop, Eunice
Sum na Milcah Chemos ni miongoni mwa wanariadha walioathiriwa na
uamuzi huo, hivyo basi watakosa mbio za Rome na Oslo siku ya Alhamisi
na Juni 11.
Rais wa Chama cha Riadha Kenya
Isaiah Kiplagat amesema hatua hiyo ya kuwazuia wanariadha hao
kushiriki michuano hiyo inalengo la kuwalinda wanariadha hao baada ya
kiwango chao kushuka.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni