Nyota wa Brazil Neymar ameonyesha
kiwango cha juu baada ya kuifungia timu yake ya taifa bao moja na
kutoa msaada wa kufunga mengine wakati Brazil ikiichakaza Panama kwa
mabao 4-0, katika mchezo wa maandalizi ya michuano ya Kombe la Dunia.
Mshambuliaji huyo wa Barcelona alipachika bao kwa mpira wa adhabu, kabla ya kumpa pande Dani Alves kufunga bao la pili katika kipindi cha kwanza.
Mabao mengine ya Brazil yalifungwa
na Hulk na Willian katika mchezo huo unaotoa picha ya namba wenyeji
hao wa michuano ya Kombe la Dunia walivyojiandaa vyema.
Matokeo mengine ya mechi za kirafiki
za kimataifa za kujiandaa na michuano ya kombe la dunia jana yalikuwa
ni Costa Rica 1 - 3 Japan, United Arab Emirates 1 - 0 Georgia, Czech Republic 1 - 2 Austria na
Switzerland 2 - 0 Peru.
Mashabiki vimwana wa Brazil wakishangilia
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni