Novak Djokovic ameonyesha makali
yake na kumtoa Milos Raonic katika michuano ya wazi ya tenesi ya
Ufaransa na kutinga nusu fainali.
Mchezaji huyo namba mbili duniani
ameshinda kwa seti 7-5 7-6 (7-5) 6-4 na kutinga nusu fainali na sasa
atakutana na Ernests Gulbis wa Lativia.
Naye Maria Sharapova alijikuta
akifungwa katika seti ya kwanza kabla ya kuamka kutoka usingizini na
kupambana vilivyo na kumshinda Garbine Muguruza na kutinga hatua ya
nusu fainali.
Mrusi Sharapova ambaye alishinda
taji la michuano hiyo mnamo mwaka 2012, alifanikiwa kumaliza mchuano
huo kwa matokeo ya seti 1-6 7-5 6-1.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni