Wachezaji wa Ivory Coast ndugu Yaya
na Kolo Toure ni Waislam
Baadhi ya nyota wa Kombe la Dunia
ambao ni waumini wa dini ya Kiislam watajikuta katika wakati mgumu
kutoathiri ufanisi wao dimbani na kuweza kutimiza imani yao ya mfungo
wa mwezi mtukufu wa Ramadhan unaotarajiwa kuanza wakati michezo hiyo
ikiendelea.
Hii itakuwa ni mara ya kwanza tangu
mwaka 1986 kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan kugongana na
michuano ya Kombe la Dunia.
Waumini wa Dini ya Kiislam huwa
wanafunga kuanzia alfajiri hadi Jioni ambapo huwa hawali chakula
chochote kwa muda huo wala kinywaji, jambo ambalo litaathiri ufanisi
wa wachezaji kadhaa wa imani hiyo huko Brazil.
Mchezaji wa Ufaransa Karim Benzema
naye ni Muislam
Mshambuliaji wa Switzerland Xherdan
Shaqiri naye ni Muislam



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni