
Mkurugenzi Mtendaji wa Mikono Business Consult Deogratius Kilawe kushoto akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu semina maalum ya uongozi bora itakayofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere siku ya ijumaa tarehe 13 Juni, anayemuangalia kulia ni msemaji katika semina hiyo Azim Jamal kutoka Canada.

Mkurugenzi wa Mikono Business Consult Themi Rwegasira akifafanua jambo kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu semina maalum ya uongozi bora itakayofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere tarehe 13 Juni, pembeni yake wa kwanza kulia ni msemaji wa siku hiyo Brian Tracy,Mkurugenzi mtendaji wa Mikono Business Consult Deogratius Kilawe(katikati) na Azim Jamal msemaji kutoka Canada.

Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Shirika la Nyumba la Taifa, James Rhombo akiongea na waandishi wa habari namna ambavyo Shirika la Nyumba limeweza kuhamasika na kuwadhamini baadhi ya wanafunzi waliofanya vizuri katika kidato cha nne ili waweze kuhudhuria semina hiyo,kushoto kwake ni Msemaji wa masuala ya uongozi na maendeleo kutoka Canada Azim Jamal.

Msemaji wa masuala ya uongozi na maendeleo kutoka Canada Azim Jamal kulia akielezea umuhimu wa semina maalum ya masuala ya uongozi kwa vijana itakayofanyika tarehe 13 Juni ukumbi wa Mwalimu Nyerere, alipokuwa akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salam, katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mikono Business Consult Deogratius Kilawe, na kushoto ni msemaji wa siku hiyo Brian Tracy kutoka Marekani.

Msemaji wa masuala ya uongozi na maendeleo kutoka Marekani Brian Tracy (katikati), akisisitiza jambo katika mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mikono Business Consult Deogratius Kilawe na kushoto ni Mkurugenzi wa Mikono Business Consult Themi Rwegasira.

Wanafunzi waliofanya vizuri katika mitihani ya kidato cha nne kwa ufaulu wa daraja la kwanza nchini amabao wamedhaminiwa na shirika la Nyumba la Taifa kuweza kuhudhuria semina maalumu ya uongozi bora itakayotolewa na wasemaji maarufu kuhusu masuala ya uongozi na maendeleo Bw.Brian Tracy kutoka Marekani na Azim Jamal kutoka Canada.

Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakifuatilia ufafanuzi uliokuwa ukitolewa kuhusu semina maalum ya uongozi itayofanyika tarehe 13 Juni ukumbi wa Mwalimu Nyerere,leo jijini dare s Salaam.
(Picha na Lorietha Laurence –Maelezo)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni