Utawala wa Jeshi wa nchi ya Thailand
umeagiza Wamiliki wa Vituo vya Televisheni kuhakikisha kuwa mashabiki
soka nchini humo hawalipi fedha ili kuona michezo ya Kombe la Dunia
inayoanza leo nchini Brazil.
Jeshi limesema uamuzi huo ni sehemu
ya kampeni ya furaha kwa wananchi wa nchi hiyo kampeni ambayo imekuwa
ikitoa huduma za bure za kukata nywele na uwepo wa matamasha ya
muziki ya bure.
Mmiliki wa Kituo Televisheni
kilichonunua haki za kuonyesha michuano ya Kombe la Dunia amedai
kutaka kulipwa fidia ya dola milioni 21.5, kutokana na uamuzi huo wa
jeshi la Thailand kutaka michuano ya kombe la dunia kuonyeshwa bure.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni