.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 30 Julai 2014

CRISTIANO RONALDO ASHUHUDIA REAL MADRID IKILALA DHIDI YA ROMA AKIWA BENCHI


Mwanasoka Cristiano Ronaldo akiwa benchi ameshuhudia Real Madrid ikipoteza mchezo wake wa kirafiki dhidi ya Roma jana usiku kwa kukubali kipigo cha bao 1-0.

Bao la Francesco Totti lililofungwa katika kipindi cha pili lilitosha kabisa kukizima kikosi cha Carlo Ancelotti kilichokosa makali ya ufungaji.

Mchezo huo ulibidi usimame kwa muda baada ya baadhi ya mashabiki kuvamia uwanjani ili kuwakaribia wachezaji wanaowapenda kuwakumbatia, kusalimiana nao na hata kupiga nao picha kwa kutumia simu zao.

               Kula hug bwana: Shabiki akijiandaa kumkumbatia Mehdi Benatia 
Shabiki  akipiga picha na Isco
Shabiki akidhibitiwa na askari

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni