Mwanaume mmoja amebainika kuwa na
virusi vya ugonjwa hatari wa Ebola huko Uingereza na kuwafanya
madaktari kuwa katika hali ya tahadhari kutokana na uwezekano wa
Ebola kuingia Ulaya.
Vipimo vya mwanaume huyo vimefanywa
katika hospitali ya Birmingham, baada ya kulalamika kuwa ana homa
baada ya kurejea Midlands akitokea Afrika ya Magharibi.
Mwanaume huyo alikuwa anatokea
Benin, kupitia Nigeria na kisha kufika Paris kabla ya kuelekea
Uingereza jumatatu na kuanza kulalamika kujisikia vibaya.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni