Kocha Louis van Gaal ameendelea
kuinoa vyema Manchester United baada ya kupata ushindi mwingine wa
penati 5-3 dhidi ya Inter Milan katika mchezo wa kujiandaa na ligi
kuu ya Uingereza uliochezwa jana Jijini Washington DC.
Katika mchezo huo ulioisha kwa sare
tasa ya 0-0, magoli ya penati ya Manchester United yalipachikwa
kimaini na Ashley Young, Javier Hernandez, Tom Cleverley, Shinji
Kagawa na Darren Fletcher.
Manchester United kwa sasa imeshinda
michezo yake yote mitatu ya kirafiki katika ziara yake hiyo ya nchini
Marekani.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni