Umoja wa Mataifa umesema kombora
lililorushwa na kifaru limeuwa wapalestina 15 waliokuwa wamehifadhiwa
kwenye shule moja inayohifadhi wakimbizi huko Gaza.
Mashahidi katika shule hiyo ya Abu
Hussein inayosimamiwa na Umoja wa Mataifa ambapo maelfu wamekimbilia
kujihifadhi, wamesema kuta zimeteketezwa na kombora hilo.
Israeli ambayo imekuwa ikilituhumu
kundi la Hamas kutumia shule kama kambi zake za kurushia makombora ya
roketi, imesema itachunguza tukio hilo.
Hadi sasa Wapalestina wapatao 1,200
na Waisraeli 55 wameuwawa tangu kuanza kwa mapigano Julai 8, mwaka
huu.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni