Kundi la Hamas la Palestina
limetangaza kutoa muda wa saa 24 kusitisha mapigano, baada ya Israeli
kuendelea na mapigano kufuatia kurushwa roketi kutokea Gaza.
Hamas ambao ndio wanamiliki eneo la
ukanda wa Gaza, wamesema usitishaji mapigano hayo utaanza muda wa saa
nane mchana kwa majira ya Palestina.
Msemaji wa Israeli amenukuliwa
akisema tangazo hilo huenda likawa ni fursa ya kusitishwa mapigano
hayo yaliyoua Wapalestina 1,060 na wanajeshi 43 na raia watatu wa
Israeli tangu Julai nane.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni