Mdhibiti wa Bajeti wa Serikali ya
Kenya Agnes Odhiambo
Magavana nchini Kenya watahadharisha
kuwa utendaji wa kaunti zao utasimama kutoka na wabunge kuchelewesha
kupitisha sheria itakayoridhia kutolewa shilingi bilioni 226.6 za
Kenya kwa ajili ya kuendesha serikali za kaunti.
Wakiongea katika mkutano na
waandishi wa habari magavana wamesema kaunti zitashindwa kulipa
mishahara ya mwezi huu kwa ajili ya huduma za afya kutokana na
kutokuwepo kwa fedha kwenye akaunti za kaunti.
Kufuatia kilio hicho cha magavana
mdhibiti wa bajeti ya serikali Agnes Odhiambo ameagiza kutolewa kwa
nusu ya fedha hizo baada ya kufikiwa makubaliano mahakamani baina ya
mabaraza ya kaunti na mamlaka ya mapato Kenya (KRA).
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni